WAPENZI wa nyimbo za zamani za taarabu asilia nchini
Jumapili hii ya Aprili 6, wanatarajiwa
kupata burudani safi na ya aina yake
kutoka kundi la Spice Modern Taarab, ndani ya ukumbi wa Regency Park Hotel,m iliyopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous
Khamsin, ambao ni miongoni mwa wadhamini wa onyesho hilo, kwa kushirikiana na
Regency Hotel, amewasihi wadau
kujitokeza kwa wingi kuufurahia kukumbushiana enzi za muziki wa mwambao wa
taarab.
Asia Idarous alisema onyesho hilo pia litakuwa ni la kila siku
ya Jumapili katika ukumbi huo ndani ya hoteli hiyo ya Regency, eneo lenye
mazingira safi na upepo mwanana huku kiingilio kikiwa cha kawaida cha sh 5,000.
“Kila Jumapili Spice Taarab watakuwa wakitoa burudani ya
nyimbo za mwambao hasa zile zilizokuwa zikipendwa, kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita usiku,”
alisema Asia Idarous.
Asia Idarous pia alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zimekuwa
gumzo kipindi hicho ni pamoja na ‘Pendo kitu cha hiari’, ‘Dunia ina fisadi’,
‘Kasha’ na nyingine nyingi. Aidha aliongeza kuwa Regency
Park itakuwa ni kiota cha burudani ya miziki hiyo ya zamani huku usiku
huo ukiwa unajulikana kama ‘OLD IS GOLD’ na watu mbalimbali wakitarajiwa
kukutana hapo na kubadilishana ya zamani
Kwa upande wa Wadhamini katika usiku huo wa taarabu asilia
ni pamoja na Times FM, Regency Park Hotel na Fabak Fashions, Pia alitoa wito
kwa wadau wengine watakao kuwa tayari kudhamini kujitokeza kuchangamkia fursa
hiyo kwa kuwasiliana na namba .0784263363 au 0713263363
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni