Kisima hiki kilichimbwa na washirazi mnamo karne ya kumi na tatu ambapo walikuja kwa Lengo la kuueneza uislamu lakini jambo la ajabu na la kushangaza ni kwamba kina urefu wa mita tatu kutoka mdomoni na kwa mujibu wa maelezo hata Mvua inyeshe kiasi gani kisima hakijai hata siku moja na hata kuwe na ukame kiasi gani maji ya kisima hiki hakikauki kamwe hata ujaze pipa sabini za maji bado mambo ni yale yale hii ni miujiza ya mungu.
Na moja ya jambo jingine ni kuwa unaweza kunywa maji haya ukanawa bali kujari wewe ni mkrisho au muislamu baraka zitakuafuata huko ulipo kwani ni maji ambayo mwenyezi mungu aliyeumba mbingu na ardhi ndiye anajua siri ya maji haya
Hapa nilikuwa najaribu kutaza jinsi mungu alivyoumba kisima ukikitazama kisima hiki uwezi kukubari kabisa na unaweza kuona kama maajabu ya mwaka lakini ndio ukweli ulivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni