Ni huzuni iliyooje kusikia simulizi ya mambo haya lakini usifanye mzaha na kama ukipata japo nafasi ya kuingia katika chumba hiki kilichpo katika uzio wa kanisa la mnazi mmoja katika visiwa vya marashi ya karafuu Zanzibar unaweza kuonja radha ya machungu ambayo wanadamu wengi hajawahi kuipata hasa wa kizazi hiki .
Lakini katika picha unayo iona hapo juu ni chumba ambacho laiti hata waharifu wakiwekwa wataipata shubiri ya mwaka kwani sio mchezo hasa siku ambazo zina hari ya joto katika kisiwa cha Zanzibar .
Chumba kilikuwa kikitumika kuhifadhia watumwa walitoka sehemu mbalimbali katika Nchi yetu au ukanda huu wa afrika mashariki
Kwa mujibu wa maelezo ya Muongoza wa wataliii anasema "
Chumba hiki unachokiona hapa kilikuwa kinatumika kwa ajili ya kuweka binadamu yaani babu zetu waliokuwa wakiitwa watumwa na walikuwa wanawekwa watumwa kama Thelathini au zaidi na unaweza kuona hari ya Chumba ilivyo na wengine walikuwa wanakufa kutokana uchovu na ukatili uliokuwa ukifanywa na watu waliokuwa wakifanya Biashara ya Utumwa" .
Katika sanamu hii unayoina hapa ni mfano wawatumwa walivyokuwa wakipangwa hakika sio jambo la kufurahia hata kwa dakika Tano lakini huu ndio uhalisia wa Biashara ya utumwa katika visiwa vya Marashi ya karafuu ambapo watumwa wengi walikuwa wakipelekwa nchi za Ulaya na Amerika .
na wakati huo watu waliokuwa wakipelekwa ulaya walikuwa wakilia kwa uchungu kuliacha bara la afrika
Lakini leo mtu akiwa anakwenda ulaya hufanyiwa sherehe ya kuagwa na kupikiwa hata ugali jambo ambalo kama wale waliofanyiwa Biashara ya utumwa wangeona imani yangu wangelaani kabisa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni