Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayojitawala katika mambo yake ya ndani. Eneo lake ni sawa na funguvisiwa ya Zanzibar iliyopo mbele ya mwambao wa Afrika ya Mashariki karibu na Tanganyika au Tanzania bara. Inajumuisha visiwa vikubwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo.
Kwa jumla ya mikoa mitano ya Tanzania imo ndani ya Zanzibar ikiwa mitatu iko Unguja na miwili Pemba. Hadi mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 sehemu hizi zilijulikana kama Usultani wa Zanzibar.
Zanzibar inatawaliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Raisi Amani Abeid Karume aliyekuwa mgombea wa CCM amechaguliwa mara ya pili na wananchi wote tar. 30.10. 2005 katika kura iliyopingwa na chama cha Upinzani CUF.
Zanzibar ina Bunge lake lenye wabunge 50 wanaochaguliwa kwa muda wa miaka mitano.
Mji mkuu na makao makuu ya serikali ni Jiji la Zanzibar ambalo liko kisiwa cha Unguja. Mji mkuu wa kisiwa cha Pemba ni Chake Chake. Idadi ya wakazi wote ilikuwa 984,625 mwaka 2002, wakiwa 622.459 wakazi wa Unguja na 362.168 wakazi wa Pemba.
Biashara ya Zanzibar ni kilimo na utalii. Mazao yanayouzwa nje ni hasa karafuu, basibasi, mdalasini na pilipili.
Jamhuri ya watu wa Zanzibar ilianzishwa baada ya mapinduzi ya 1964 iliyomaliza Usultani wa Zanzibar. Rais wa kwanza alikuwa Abeid Amani Karume hadi 1972 aliyefuatwa na Aboud Jumbe (1972-1984). Rais wa tatu aliyemfuata alikuwa Ali Hassan Mwinyi (1984-1995) aliyeendelea kuwa pia rais wa Tanzania tangu 1985.
Rais na mwaka 2000hadi 2010 Amani Abeid Karumeambaye ni mwana wa rais wa kwanza. na Rais anayeongoza sasa ni Dk Ali mohamed shein ..
Historia inajionesha ya kwamba kiasi cha miaka 20,000 kumekuwepo
makazi ya binadamu katika visiwa vya Zanzibar. Visiwa hivi ni sehemu ya
kumbukumbu ya kihistoria ya ulimwengu wakati waajemi wafanyabiashara
waliigundua na kufanya ndio makao makuu kwa safari kati ya Mashariki ya
Kati, India, Na Afrika.
Katika karne ya mwanzo AD Zanzibar pamoja na mwambao wa Afrika ya
Mashariki ulikua katika ufalme wa Saba,Katika kipindi cha karne ya 3 na
4AD,Wabantu walianza biashara na Waarabu waliokuja Afrika ya Mashariki.
Katika karne ya 7 AD,waarabu walikuja Zanzibar kibiashara pia kusambaza
Dini ya Kiislam,Waarabu ndio waliyoipa jina ZANZIBAR kutokana na neno la
Kiarabu ZINJI BAR yaani sehemu ya watu weusi.
Lugha ya kiswahili imeanza kutumika kiasi cha karne ya 13 AD,Lugha ya
kiswahili ilitokana na kuchanganyika lugha ya kiarabu na lugha za
kiafrika.
Karne ya 16 AD wareno walikuja Zanzibar lakini utawala wao ulifuatiwa
na kutokuwepo utulivu,lakini biashara ya Utumwa iliwaweka watu pamoja.
Waarabu kutoka Oman walichukua utawala Zanzibar katika karne ya 17 AD,Na
Zanzibar ilikua ni makao makuu ya utawala wa Waomani.
1820-1870 Zanzibar ilifaidi matunda mazuri ya kiuchumi na maendeleo
yaliyosababishwa na utawala wa kisultani na hivyo kupelekea Zanzibar
kuwa na mwakilishi nchini marekani na kupelekea kuenea kwa Dini ya wa
kiislam. Katika karne ya 19 AD Zanzibar ilikua chini ya utawala wa
Oman,mwaka 1830 Zanzibar ilikua inaongoza kwa kilimo cha karafuu ,na
hiyo kupelekea mahitaji ya watumwa kuongezeka kutumika katika kilimo.
1885 kamisheni kutoka Uengereza na Ujerumani iliamua kuigawa Zanzibar
kutoka katika utawala wa Kisultani na ndio ulikua mwisho wa utawala wa
kujitegemea kwa Zanzibar na mnamo mwaka 1886 sultani alikubali
maridhiano hayo.
1890 Zanzibar ilikua chini ya uangalizi wa waingereza rasmi lakini
uchaguzi wa mwanzo ulifanyika mwaka 1957,na miaka iliyofuata kukakuwepo
fujo na machafuko kutoka kwa waafrika wanaodai uhuru dhidi ya utawala wa
kiarabu. Mwezi wa 12 mwaka 1963 Waingereza waliipa uhuru Zanzibar chini
ya jumuiya ya madola,na mwezi wa mwaka 1964 Zanzibar ilifanya mapinduzi
kujikomboa kutoka katika utawala wa kisultani,muda mchache baadae
iliungana na Tanganyika kuunda Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA.
Idadi ya Watu
idadi ya Watu na Makazi.
Watu wa Zanzibar ni wa asili mbalimbali, hasa watu wa asili ya Afrika
Bantu[17]; Waasia, awali kutoka India na nchi za Kiarabu. Idadi ya
wakazi wa Zanzibar ilikuwa 984,625 mwaka 2002,[18] tarehe ya sensa ya
mwisho, kwa kiwango cha ukuaji wa 3.1%, . Hii, karibu theluthi mbili ya
watu - 622,459 - wanaishi Kisiwa cha Zanzibar(Unguja), Mkoa wa mjini
magharibi ndio wenye idadi kubwa ya wakaazi kiasi cha watu 205,870.
Pemba ina jumla ya makazi sawa. Mji mkubwa ni Chake Chake, na idadi
ya 19,283, mengine ni Wete na Mkoani. Kuna tofauti kubwa katika kiwango
cha maisha kati ya wakazi wa Pemba na Unguja na kati ya wakazi wa mijini
na vijijini. Wastani wa mapato ya kila mwaka ya US $ 250 na ukweli
kwamba karibu nusu ya maisha ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa
umaskini. Huduma ya afya vifo vya watoto wachanga bado ni 83 katika
Waliozaliwa 1000 , na inakadiriwa kuwa utapiamlo huathiri moja katika
tatu ya watu wa visiwa ', matarajio ya maisha wakati wa kuzaliwa ni 48.
Wakati matukio ya VVU / UKIMWI ni ndogo mno kwa Zanzibar kuliko Tanzania
kwa ujumla (0.6% ya idadi ya watu, kama dhidi ya wastani wa kitaifa
wa%8).
Dini
Dini ya Uislamu ni kiasi cha 97% . Mchanganyiko iliyobaki ni mchanganyiko wa Hindu na wa kikristo.
Dini za kihindi pia zipo katika visiwa hivyo, lakini wengi wao
walikimbilia nchi au kuuawa wakati wa mapinduzi ya 1963. Wakristo
walikuja baadaye wakati wa kipindi cha utawala wa Kireno na ukoloni wa
Uingereza.
Kuna misikiti 51, ambaye waadhini hugongana kwa kila mmoja wakati wa
maombi, pamoja na Majumba ya Hindu sita mahekalu na Kanisa Kuu Katoliki
kama vile Kanisa Kuu Anglican katika mji wa Zanzibar Stonetown).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni