Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno.
Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya
matumaini mema Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu
la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao
wa Afrika.
Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499
walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji
wa Zanzibar. Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli
za Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la
mwambao. Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na
Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba. Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na
bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la
kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman. Jeshi hili la Oman
inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwanga
Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.
Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi
kuwaka moto mji wa Mombasa, Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini,
mbali na mafikio ya mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo
za miongo za jahazi (waarabu). Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman
Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo
alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu. Malezi
yake katika maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote
kuviendeleza visiwa hivyi vyenye ustawi. Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar
kama kama ni Oasisi katika bahari. Alisimamia mipango mikubwa ya upandaji miti,
alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha
mamia ya wageni. Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi.
Na alijua kwamba biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa
litaimarishwa kwa vitu na mambo mengine pamoja na usalama. Vile vile alitarajia
na kutambua kwamba angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za
kibiashara zitakazo endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa
hivyi. Aliwakaribisha na kuwaomba wafanyabiashara kutoka India kufungua matawi
ya ofisi zao ndani ya Zanzibar ili kuimarisha biashara. Wafanyabishara hawa
wengi kutoka India walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya
kutekwa India na Uingereza. Kwa maana hiyo, alianza kuwakaribisha maofisa wa
kiingereza visiwani ili kuwakilisha maslahi ya raia hawa wahindi wa kiingereza.
Mara tu tena baadae alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na
Serikali ya kiingereza na Serikali nyengine za Magharibi.
Majengo ya biashara yalijengwa ndani ya Mji Mkongwe na
Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na Kiingereza. Bandari ya
Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia matengenezo Meli za kivita na
vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara. Meli hizi zilileta mapote ya ziada ya
watu wa magharibi ndani ya Zanzibar. Kama ni makaribisho mema ya wageni wengi
katika Oasisi yake. Sultani aliruhusu watu wa imani zote kuendesha shughuli zao
za kidini walivyopenda.
Akiwa Muislamu mwenye imani kamili, Sultani alionyesha mfano
bora wa uvumilivu juu ya mahitajio ya kidini ya watu wengine. Wakati huo huo
akijenga furaha na imani katika dini ya mababu zake, kwa bidii zote. Warithi
wake alifuata utaratibu wa Sultani Seyyid, wakiruhusu kuanzishwa mahekalu mengi
tu ya kihindi, makanisa mawili, moja la kikatoliki na kiprostanti, sehemu za
kimazishi za zoroastriani na misikiti kwa kila dhehebu kuu au dogo la kiislamu
ndani ya mji mmoja. Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa
ndio waliobakia Zanzibar. Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada
lakini waliweza kuifanya hai jumuia yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi.
Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha
wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara chache na
wachungaji katika meli bandarini. Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo
zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri
Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya
kimisheni ya kanisa la kiingereza (English Church Missionary Society).
Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache mbeleni walitoa
kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi kuanzisha kanisa ndani ya
visiwa hivyi.
Ukuwaji wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza
ulishajiisha raghba ya wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David
Livingstone aliyoitoa mwaka 1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na
wafanyakazi Afrika. David Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa
utakuwepo tu kupitia biashara na ukiristo. Baadae Livingstone alitumia siku
nyingi tu Zanzibar ambao alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.
Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa
Afrika ya Kati (UMCA). Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni
mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and
Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham
na Dublin. Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni Askofu wa
Afrika ya kati na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea
huko Afrika ya Kati.
Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA)
lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya
Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi. Kwa
ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa
nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi
ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika
katika sehemu iliyojulikana kama Magomero.
Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari ya
jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo
yake. Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea
kufa kwa askofu. Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya
kipindi
cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana
na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo
halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea
na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa. Askofu
mpya, George Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya
mtiririko wa mto kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu
liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa
kwa miezi hivi tu.
Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa
yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA)
waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika
kati kati ya Afrika. Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha
Johanna, maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar
ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano,
upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.
Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar
tarehe 31/08/1864.
Ujumbe huu ulipowasili ulipokewa na wamisionari wakatoliki
wa Kifaransa. Wamisionari wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya
miaka minne kabla ya wamisionari wa kiingereza. Katika mwezi Septemba mwaka
1860 Abbe Favat ambaye alikuwa Mfaransa mdini maarufu mwenye nguvu alitiliana
mkataba na Seyyid Said kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake
katika Kisiwa cha Reunion na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake
cha mapadri wawili wasio watawa na watawa sita wa kike (Filler de Marie)
walikuwa wakiishi katika makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo
hapo Shangani. Jengo hili la watawa linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860,
lakini ujenzi huu inawezekana ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba
iliyokuwepo kabla. Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza
lililojengwa Zanzibar kwa miaka 200.
Ruhusa iliyotolewa na Sultan Majid kwa Wafaransa hawa
kuanzisha duka ndani ya Zanzibar ilitafsiriwa kama ni juhudi za Sultani za
kuweka uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nao Waingereza Zanzibar kwa
kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa kizungu. Ikiwa ushindani wa kisiasa ndio
uliompelekea Sultan Majid za kukaribisha pamoja matawi tofauti ya wamisionari
wakiristo hata hivyo matokeo hayakuwa hayo kwani kwa upande wa wamisionari hawa
hakukuwa na msuguano wowote. Mahusiano yao mazuri makundi hayo mawili ya
wamisionari ulitokana na ukweli kwamba Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
wa kianglikana (UMCA Anglicans) ulikuwa ni ujumbe wa watu watukufu ambao wenye
mafunzo ya kikatoliki ya kiengereza (Anglon Catholic Learnings)
Wamisionari wakifaransa walikuwa makini kuepuka matatizo
yoyote Zanzibar kwa kutambua uhalisia wa maisha ulivyo ndani ya nchi ya
kiislamu ya Zanzibar, Wafaransa kuanzia 1862 wafuasi wa Holy Ghost Order,
waliamua kujikita katika maeneo maalum kama ya elimu, shughuli za uchungaji kwa
jumuia ndogo ya mjini ya magoa wakatoliki na huduma za afifu na walifungua hospitali
ya mwanzo iliyopendekezwa na Sultani ya kizungu. Kwa hili waliojenga maoni
mazuri kwa warabu.
Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibar hawa kidogo
hawakuwa na azma yoyote kufuata imani ya wageni hawa wapya. Wamisionari wa
kikatoliki walilielewa hili lakini waliamini kwamba kundi kubwa la wafuasi
wapya wa dini hii ya kikiristo litaweza kupatikana masafa machache kuvuka
mlango bahari wa Zanzibar huko Tanzania Bara. Walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo
katika mwambao wa Tanzania Bara katika mwaka 1868 na kwa sehemu kubwa walitumia
nafasi walizonazo Zanzibar kama ni makao makuu ya kuzidisha harakati zao
Tanzania Bara. Harakati hizi ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Kifaransa ndani ya
Bagamoyo.
Hospitali ya
Kifaransa ndani ya Zanzibar ilijengwa mkabala na jengo la watawa. Hospitali
ilimalizwa kujengwa na kuanza kazi kufikia mwaka 1890. Kipindi hicho wakatoliki
walien delea kutumia uhusiano mzuri na majirani zao wa Zanzibar, wakipata
ruhusa ya kujenga kanisa la mtakatifu Joseph katika mwaka 1894. (Cathedral of
Saint Joseph in 1894). Jiwe la msingi la kanisa hili kuu liliekwa tarehe 10
Julai 1896. Misa ya mwanzo katika kanisa hili kuu jipya iliendeshwa na Askofu
Allegeyer katika usiku wa krismas 1898.
Kadri ya wakati ulivyokuwa ukienda, hospitali hii ya Zanzibar
ilipungua umuhimu wake na jengo hilo likafanywa kuwa ni skuli. Hii ilikuwa ni
skuli ya kitawa ya mtakatifu Joseph (St. Joseph Convent School).
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
(UMCA) hawakuzubaa katika kipindi hichi. Akianzia kwanza kuishi katika nyumba
Mambo Msiige, katika eneo la Shangani, ambapo haikuwa mbali na ujumbe wa
Kifaransa, Muingereza mchapa kazi shupavu alianzisha ustawi wa majengo ya
ukubwa wa kuvutia na ya aina tofauti. Kwanza walinunua sehemu ya ardhi ya kilimo
Kiungani pembezoni mwa mji wa Zanzibar Kaskazini. Ujenzi wa bweni kwa ajili ya
vijana watumwa walioachiwa huru uliendelea katika eneo hilo kufikia mwaka 1866.
Karibu ya hapo mava sehemu ya kuzikia ilianzishwa, na hadi leo mava hii inayo
baadhi ya mabaki ya wakiristo wa mwanzo wa Zanzibar.
Baadae ilinunuliwa ardhi nyengine katika mwaka 1873, ardhi
hii ilikuwa karibu na kitovu cha mji ambalo ni jengo kubwa zima la mjini ambalo
liliwahi kuwa uwanja wa soko kongwe, ambapo watumwa walikuwa wakiuzwa, Mara
wito ulitolewa wa fedha kusaidia ujenzi wa kanisa katika eneo hilo ambao uovu
huo wa biashara ya utumwa ulifanyika. Huu ulikuwa mwanzo kanisa kuu la kristo
(Christ Church Cathedral).
Mwaka uliofuata Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati
(UMCA) walinunua ardhi ya kilimo Mbweni kusini mwa mji karibu na bahari.
Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya kati
(UMCA) walipanga kujaza milki zao kwa majengo ya kidini na yasiyokuwa ya
kidini. Katika mwaka 1882 walianzisha ujenzi wa kanisa la parokia la mtakatifu
John (St. Johns Parrish Church) huko Mbweni. Karibu ya kanisa hilo walijenga
kijiji na shamba dogo kwa ajili ya waliokuwa watumwa zamani na pia walijenga
Makaazi ya watoto wadogo wa kiume wa kilimani, ambayo baadae iligeuzwa skuli ya
wasichana. Huko Mbweni walijenga karakana nyingi tu za elimu amali kwa ajili ya
kuwafunza wafuasi wapya wa dini stadi muhimu na baadae kuwa Chuo cha kidini cha
Mtukufu Mark, ambacho baadae kilihamishiwa kiungani.
Jiwe la msingi la kanisa kuu la ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika
ya Kati (UMCA Cathedral) liliekwa mwaka 1873 katika siku ya siku kuu ya krismas
katika eneo la mjini. Uwanja wa soko kongwe ulianza kujazwa majengo ya ujumbe
wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati.
Jumba la Mkunazini lilijengwa katika mwaka 1875 na kanisa mara
baada ya kujengwa jumba la kunazini lilihamisha makao makuu yake kutoka Mambo
Msiige na kuwa Mkunazini. Zahanati ilijengwa katika mwaka 1877, hatimae
iligeuzwa kuwa hospitali yenye kutoa huduma kamili katika mwaka 1893. Skuli ya
Mtakatifu Mon`ica, nyumba ya kasisi mkuu na Askofu ilijengwa katika uwanja wa
soko kongwe. Jengo hilo la skuli ya Mtakatifu Monica bado mpaka leo linatumika
kama ni hostel/dahalia Mtukufu Monica.
Mwenye kustahiki sifa ya mafanikio haya ilikuwa hakika ni
kanisa kuu la kristo. Mradi usio wa kibiashara ambao ulisimamiwa binafsi na
Askofu wa tatu wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati Edward Steere,
utabakia kuwa moja ya mifano ya kuvutia na bora wa usanifu majengo ndani ya
Afrika uliofanywa na wakiristo wa mwanzo.
Wakati eneo lake lilijazwa na haiba nzuri ya shinikizo la
kidini, ukaribu wake na kijito kidogo chenye manukato ilisababisha baadhi ya
watu kutia wasiwasi juu ya athari zake kwa afya za wamisionari. Kijito hicho
kidogo ambacho kilitambulika kama ni mfano wa mfereji wa venice huko Italy
(Venetian Canal) kwa maelezo ya kikanisa kilikuwa kiukweli hasa ni topetope
zenye kunuka wakati wa kupwa kwa maji. Eneo hili liliacha kutoa moshi wenye
kunuka na kudhuru katika miaka ya 30 (30s) baada ya kijito hicho kufunikwa na
barabara, moshi ambao uliendelea kujitokeza kwa masiku wakati wa kujaa na kupwa
maji.
Haiba binafsi ya ushiriki katika ujenzi wa Daktari Steer
unaweza kuonekana na wengi juu ya mabadiliko aliyoyafanya kwa ramani
zilizoletwa kutoka Uingereza na juu ya majaaliwa ya nguzo za mawe ambazo
husimamishwa karibu na nyuma ya ukumbi wa kanisa. Nguzo hizi zilitiwa kipindi
ambacho Askofu alikuwa safarini Tanzania Bara kwa kazi za kanisa. Kwa hivyo,
utiaji huo wa nguzo hizo ulikosa usimamizi wake. Wafanyakazi hao walizitia nguzo
hizo kwa kusimamisha wima kama alivyoelekeza Askofu lakini kwa bahati mbaya
walizigeuza juu chini juu. Baada kurejea Askofu alizichunguza na kuamua zibakie
kama zilivyo,kama zinavyoonekana leo. Hii ilitokana na azma yake ya
kushindikiza kazi iendelee bila ya kurudi nyuma.
Thamani hasa kubwa ya juhudi zake za usanifu majengo ni Paa
la kanisa kuu. Akikumbuka matokeo yasiopendeza wakati akijaribu kufanya
matengenezo la paa lililooza la kanisa lake kongwe la Kiingereza, Askofu Steer
alidhamiria kujenga paa kwa kutumia muda mrefu.
Aliamua kujenga paa la zege badala ya kutumia mbao kwa
sababu ya kuhofia mbao hizo kuharibiwa na mchwa na hatari ya moto na hakuweza
kujenga paa hilo kwa kutumia vifaa vya chuma kwasababu hakuwa na fedha ya
kugharimia.Alitumia vifaa vya kienyeji katika ujenzi, alichanganya saruji na
kokoto katika juhudi zake za kujenga paa kubwa lenye upana wa futi 28.5.
Ilikuikamilisha kazi hii alitumia mbea moja ya chombo kilicotengenezwa
Uingereza mbacho kililetwa hali ya kuwa hakijaunganishwa pamoja. Mashine hii
iliekwa kwenye eneo la ujenzi ikiwa na viringi vilivyotiwa ili kuweza
kuzungushwa zungushwa kutoka sehemu moja kwenda nyengine pale ambapo kipande
kimoja cha paa kinapomalizika kutiwa. Pale ambapo muhimili unapotaka kuondoshwa
kundi kubwa la watu ilibidi kukusanyika pamoja. Mkusanyiko huu wa watu unakuwa
unatweta wakati vifaa vya kujengea jukwaa vinabomolewa, na huachwa kushangaa na
kidogo na kukata tamaa pakiwa hapakutokea lolote. Paa ambalo watu wote
hawakutegemea kuchukua muda bila ya kuanguka sasa limeweza kubakia zaidi ya
karne moja/miaka 100.
Mfalme ambae kwa wakati huo alikuwa Seyyid Barghash
alivutiwa sana na aliamua kutoa saa kubwa, ili kuupamba mnara wa kengele ambao
uliwekwa pembe ya kusini magharibi ya jengo. Kwa bahati mbaya haikuwepo saa
katika ramani ya mwanzo. Uamuzi wa busara wa kisiasa kupokea na kuiweka zawadi
ya Sultani ulipelekea marekebisho kufanywa juu ya mnara na kuufanya mwembamba
na mrefu zaidi. Uamuzi huo kwa upande mwengine uliathiri pia zawadi zawadi
nyengine ya seti nzuri ya kengele 25, seti za mlio wa saa ambazo ziliweza
kupiga milio mirefu. Hata hivyo ukubwa na uzito wa seti hizo ulikuwa hauwezi
kubebwa na mnara huo mwembamba. Kengele 13 tu zilitiwa kwenye mnara huo na
kengele zilizobakia zilitawanywa kwa makanisa mengine na maskuli.
Wakati shughuli zote hizi zikiendelea katika kisiwa mama,
wamisionari kutoka jumuia ya kirafiki ya kidini, the Quakers walianzisha
makaazi karibu kabisa na kisiwa cha Pemba. Quakers walifika Zanzibar mapema
kufikia mwaka 1865, wakati huo walikuja kama ni waajiriwa wa kampuni za
kibiashara za watu wa Magharibi. Lakini Juu ya hivyo, mpaka ilipofikia tarehe
20/Januari/1897 ndipo ujumbe wa kudumu wa Quaker ulianza mahala panapoitwa
Banani ambapo ni karibu na kitivu cha ghuba ya Chake Chake mwambao wa Magharibi
ya Pemba.
Kama vile ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati, kichocheo
cha fedha kwa ajili ya ujumbe wa Pemba zilitokana na raghba za vita dhidi ya
utumwa alizokuwa nazo kila Quaker. Kuanza hapo tena baadae utumwa ulipigwa marufuku
rasmi katika visiwa hivyi ingawa maisha ya wengi waliokuwa watumwa kabla
hayakubadilika.Kwa wale watumwa waliohama katika maeneo ya wale waliokuwa
wakiwamiliki walikosa makaazi ya kuishi na hofu kubwa ilienea juu ya kuwepo
vikundi visivyofuata utawala wa sheria vikizunguka zunguka sehemu za ma
shambani.
Ujumbe wa Quaker, kwa maana hio ilibidi uwe ujumbe Chapakazi
ili watumwa walioachiwa huru waweze kupata kazi na kusoma biashara. Kiongozi wa
ujumbe huu Theodore Bartt bila hata ya kufika Pemba, alisema katika ukumbi wa
mkutano ndani ya Uingereza Ni jambo mwafaka na sahihi kwake yeye mtu alieachiwa
huru kumiliki shamba kubwa ndani ya Kisiwa hichi na kuonyesha dunia/ulimwengu
kwamba watu walioachiwa huru watafanya kazi kwa bidii na uaminifu na kuwa wastahamilivu
na kujitahidi kujenga maisha yao."
Theodore Buft aliamini kwamba biashara na ukiristo ilikuwa
ndio njia ya uongofu na kuweza kuweza kuelimika.
Watumwa na Waliobadili Dini
Ujumbe wa Quaker kwa Pemba ulikuwa ni mlolongo wa karibu
zaidi wa wakiristo wa uasisi wa Mji huru ndani ya Afrika ya Mashariki kwa ajili
ya makaazi ya watumwa walioachiwa huru. Kwa miaka, jeshi la majini la kifalme
walileta makundi kwa makundi watumwa kwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya
waliowakamata kutoka bahari kuu. Watu hawa walioachiwa huru walikuwa rahisi
kwao kugeuzwa na kuwa wakiristo na kwa kweli wengi katika wao waligeuka kuwa
wafuasi wa dini ya kikiristo.
Lakini juu ya hivyo, wingi wa wakiristo hawa wapya na
mahitaji yao maku bwa yalikuwa ni changamoto kwa raslimali na subira ya
wafadhili wao. Wakiangalia demografia wamisionari waliona njia pekee ya
kuwahudumikia wakiristo wapya ni kuanzisha chimbuko la Padri wa kiafrika.
Kwa hivyo wote wakatoliki na waprotestanti walifanya bidii
kuwajumuisha makundi ya kienyeji shughuli na mambo ya kanisa na hii yote
ilipelekea kujua na kufunza mtumishi bora kwa ajili ya kuendesha shughuli za
kidini.
Kwa Zanzibar harakati zote hizi zilikuwa katika eneo la
Kiungani ambapo kwanza ilianzishwa dahalia kwa watumwa vijana walioachiwa huru,
na baadae Chuo cha Mafunzo ya ualimu cha Mtakatifu Andrew na baadae Chuo cha
kidini/theolojia kila moja kati ya hivyo kilijaribu kuwafunza na kutathmini
matokeo ya vijana wa kiafrika. Kiasi cha wanafunzi 50 kwa kipindi kimoja cha
wakati waliishi na kusoma Kiungani. Mitaala ilisisitiza heshima, elimu, imani
na michezo. Wanafunzi wazuri walifanywa kuwa walimu na wanafunzi bora kuliko
wote walifanywa kuwa mapadri.
Jambo moja la kuvutia juu ya michezo iliyoanzishwa kwa ajili
ya wanafunzi wa Kiungani ni kwamba ilifanya baadhi ya mashindano ya kwanza ya
timu mjumuisho ndani ya Afrika. Timu hiyo ya skuli mara walicheza dhidi ya
makundi ya mabaharia wazungu. Mchezo wa Kriketi ulianzishwa mwanzo katika mpira
wa miguu lakini hata hivyo mchezo wa mpira wa miguu ulipendwa zaidi kwani
makundi kwa makundi ya watu walikuwa wakikusanyika kuangalia mpira wa miguu.
Inaaminika kwamba kanisa iliendeleza michezo kusaidia kuwafunza waafrika
maadili mapya ya jumuia, ufuataji wa sheria, kuweka wakati, kufanyakazi kwa
pamoja na mashirikiano na maofisa husika. Wanafunzi wa kizanzibari walicheza
mechi/michezo hii kwa hamu na raghba na umahiri wao wa mchezo wa mpira ulijenga
mshangao na fadhaa kwa wapinzani wao. Lakini lisilosahaulika zaidi
walilojifunza ni kwamba wao wanaweza kufanikiwa katika mchezo wowote na sio
mpira wa miguu tu.
Kwa maelezo na taarifa zaidi juu ya wamisionari wa mwanzo
Zanzibar. Napendeleza soma kitabu kipya chenye kichwa kilichoandikwa Zanzibar,
May Allen and the East African Stave Trade ( Biashara ya Utumwa ya Afrika
Mashariki na May Allen Zanzibar), kilichoandikwa na Yoland Brown.
May Allen alikuwa ni nesi wa mwanzo wa ujumbe wa Vyuo Vikuu
kwa Afrika ya Kati aliwasili katika mwaka 1875 na alifanyakazi Zanzibar kwa
kiasi cha miaka 12 hasa katika sehemu ya Mkunazini. Maelezo yake kupitia barua
zake nyumbani zilivuta ari na dhamira kwa payonia hawa wa mwanzo. Kitabu hiki kimefanyiwa
utafiti wa kina na kuandikwa vyema, kwa kweli kitabu hiki ni kumbukumbu bora
kabisa ya historia iliyokaribia kusahaulika kabisa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni