MUZIKI WA MALIMBA

MUZIKI WETU

HABARI? MPENZI MSOMAJI KARIBU KATIKA KURASA HII MAALUM KWA AJIRI YA HABARI ZIHUSUZO UTALII NA UTAMADUNI KUTOKA KATIKA VISIWA VYA MARASHI YA KARAFU ZANZIBAR ,NA MAENEO JIRANI YANAYOFANANA TABIA NA VISIWA HIVI +255 713 15 33 48

Ijumaa, 10 Januari 2014

MNARA WA MAPINDUZI KUVUTIA WATARII ZANZIBAR



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema mpango wa Serikali hivi sasa ni kuimarisha maeneo ya biashara katika mji wa Zanzibar sio tu kwa lengo la kuimarisha huduma za biashara lakini pia kuupa mji huo haiba bora zaidi ili uzidi kuvutia wageni.Dk. Shein ameeleza hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar unaojengwa katika eneo la Michenzani lililopo katikati ya mji wa Zanzibar.


Amesema Ujenzi wa Mnara huo ambao utakuwa na huduma mbalimbali utaungana na mradi wa kuendeleza eneo jirani hapo Michenzani ambalo limepangwa kujengwa sehemu mpya za biashara ambayo itajumuisha maduka makubwa na majengo ya ofisi.Alibainisha kuwa mnara huo umejengwa katika eneo la Michenzani ambalo limebeba historia kuanzia ya ujenzi wa mwazo wa mji wa watu masikini mjini Unguja, harakati za kuwaunganisha wananchi wa Zanzibar kwa ajili ya mapambano dhidi ya ukoloni pamoja na kuwa mfano wa utekelezaji wa ahadi za Chama cha Afro Shirazi za kuwapatia wananchi makazi bora.

Katika hotuba yake hiyo kwa mamia ya wananchi waliohudhria hafla hiyo Dk. Shein alieleza pia mpango wa Serikali wa kujenga kituo kikubwa cha Biashara katika eneo la Darajani ambalo huko nyuma lilikitumika kama kituo cha daladala.Aliwaeleza wananchi kuwa maeneo kama hayo ni muhimu katika kuendeleza biashara za wajasiriamali nchini na kutolea mfano mafanikio waliyoyapata wajasiriamali wanawake katika kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo alisema zinahitaji maeneo bora ya kufanyia biashara ambayo ni rahisi wateja kuyafikia.

Kwa hiyo aliwataka wafanyabiashara na wananchi kuunga mkono hatua hizo za Serikali ambazo zimedhamiria kuboresha mazingira na kuongeza fursa kwa wananchi kufanya biashara hivyo kuufanya mji wa Zanzibar kuzidi kuvutia wageni wengi ndani na kutoka nje.Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Dk. Shein aliwakumbusha wananchi kuzingatia malengo na shabaha za Mapinduzi ili kuyaenzi na kuyadumisha.

Alibanisha kuwa malengo la Mapinduzi ni kuleta ustawi wa jamii pasi na ubaguzi wa aina yeyote kwa watu wote na shabaha yake ilikuwa ni kuishi kwa amani, utulivu na mshikamano baina ya watu wote wa Zanzibar.Kwa hiyo alisisitiza kuwa kuendeleza amani, utulivu na mshikamano iwe ni suala linalopewa kipaumbele na wananchi wote bila ya kujali tofauti za vyama kwa kuwa hayo ndio msingi wa maendeleo yaliyofikiwa na kwa utekelezaji wa mipango mikuu ya maendeleo ya nchi.

Amesema kuwa ni lazima wazanzibari wakubaliane kuwa masuala hayo ni ya msingi bila ya kujali tofauti zao na kusisitiza kuwa utulivu uliopo sasa umesaidia kuvutia washirika wa maendeleo kuisaidia Zanzibar na kutahadharisha kuwa kinyume chake washirika hao hawatafanya hivyo.

Dk. Shein alibainisha kuwa nchi kuwa na kitu cha kumbukumbu ya historia au utambulisho wake si kitu kigeni hivyo ujenzi wa Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi umelenga kuweka historia ya ukombozi wa Zanzibar kama ambavyo watu wa nchi nyingine walivyofanya kuenzi historia za nchi zao.

Akitoa maelezo ya ujenzi wa mnara huo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Dk. Khalid Mohamed alieleza kuwa mnara huo unaojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar-ZSSF utaendeshwa kibiashara na kuwa chini ya Mfuko hadi utakaporejesha gharama zake.Taarifa hiyo ilieleza kuwa ZSSF mbali ya kujenga mnara huo itatengeneza pia bustani na kuweka vifaa vya kuchezea watoto katika eneo la mnara pamoja na kujenga majengo mpya ya biashara katika eneo linaloangaliana na eneo hilo upande wa pili wa barabara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni