Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuomba Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil ,Barcelona na Chelsea kusalia Nchini kwa Siku Kadhaa ili Apate Nafasi ya Kwenda Kutizama Vivutio Vya Utalii Vilivyopo Hapa Nchini .
Rais Samia Ametoa Ombi Hilo wakati wa Akipokea Kombe Halisi la Dunia linalofanya Ziara ya Siku mbili ikiwa ni Kiashiria cha Hamasa la Kombe la Dunia litalofanyika Nchini Qatar Mwezi November Mwaka Huu ambapo hii ni Mara ya pili kufanya Ziara Hiyo Mara kwanza lilipokewa na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu Nne Jakaya Mrisho Kikwete .
Rais Samia Amemwambia Belleti '' Belleti you can spare some Days to Visit Serengeti so That you can see the wonders of Tanzania .
Akimwambia Kuwa unaweza Kusalia hapa Nchini kwa siku Kadhaa ili ujionee Maajabu ya Vivutio vya Utalii vya Tanzania kwani Ukitoka na Kurudi tena Gharama zinaweza kuwa Kubwa .
Julioni Belleti ambaye Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ni Moja kati ya Wachezaji waliokuwemo Kwenye Kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil kilichotwaa ubingwa kwa Mara tano katika Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika kwa Mashirikiano kati ya korea ya Kusini na Japan 2002 .
Pia amewahi Kutwaa Ubaingwa wa Ulaya akiwa na klabu cha Barcelona cha Uispani na amewahi Pia Kucheza katika Klabu cha Chelsea kinachoshiriki ligi ya kuu ya Nchini uingereza .
Aidha Rais Samia amegusia mambo mbalimbali Ikiwemo kuongeza bidii katika Maandalizi ya timu za Taifa ambazo serikali imekwisha Aanzisha mfumo Maalumu wa Timu ya Taifa ya Tanzania .
Kikombe Hicho kinazuru Nchini Nane katika Bara afrika katika Hizo Nne hazijafuzu kucheza kombe hilo la Daunia .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni