Moja
kati ya mambo mengi na ya msingi katika miaka ya leo ni watu kufanyiwa maziko
ya kifahari kanakwamba vitu wanavyokwenda kuzikwa navyo watavitumia
huko waendako na wengine wamekuwa wakilaani utaratibu huo kutokana na imani zao
binafsi na maisha ya kileo lakini kumbe
tabia hii haikuanza katika karne ishirini na moja imeanza katika karne ya kumi
na tano miaka takriban mia tano na ushehe hivi imepita ambapo jamii za wakati
huo zilikuwa zikifanya haya yanayofanyika leo.
Leo tunamtazama Binti wa Kishirazi aitwae Mwanamwali Binti
huyu aliposwa katika Karne ya Kumi na tano na hakuna ushahidi wa moja kwa moja
wa Binti huyo alikuwa na Umri wa Miaka Mingapi katika maisha yake ya kuishi
Duniani Kaburi la mwanamwali lipo katika Kijiji cha Kunduchi pwani kijiji
ambacho kinahistoria kubwa zaidi ya Uislamu.
Mwanamwali Baada ya kuposwa alifariki Dunia siku chache
baadae na ndoa yake haikufungwa japokuwa mahali ilikuwa tayari imekwisha
kutolewa kwanini Mwanamwali ? Kaburi la
Binti huyu wa kishirazi limejengwa kwa mawe ya matumbawe ambayo hata leo bado
yapo Tangu karne ya Kumi na Tano kikubwa zaidi na cha ajabu ni kuwa waliamua
kuweka vitu alivyolipiwa kama mahali wakati anaposwa ambapo vimegandanishwa kwa
kutumia chokaa ya moto na vipo hadi leo hii, ni kaburi lililojengwa mfano wa
Nyumba na limerembwa utadhani kulikuwa na mashine za kufanyia kazi hiyo wakati huo .
Hii ni moja kati ya historia kubwa ambayo ipo kunduchi chuo
cha Uvuvi ambapo watu wengi hawaitilii maanani pengine kwa kutojua umuhimu au
maana ya historia za aina hii na kuna vitu vingi sana vya kustaajabisha katika
makuburi haya pengine inawezekana yakawa
ndio makaburi yenye Gharama zaidi kuliko hata ya sasa kiuhalisia Tabia hizi
zimekuwa zikijirudia rudia katika maisha ya wanadamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni