MUZIKI WA MALIMBA

MUZIKI WETU

HABARI? MPENZI MSOMAJI KARIBU KATIKA KURASA HII MAALUM KWA AJIRI YA HABARI ZIHUSUZO UTALII NA UTAMADUNI KUTOKA KATIKA VISIWA VYA MARASHI YA KARAFU ZANZIBAR ,NA MAENEO JIRANI YANAYOFANANA TABIA NA VISIWA HIVI +255 713 15 33 48

Jumatatu, 21 Septemba 2015

MSHIRAZI ALIEFIA KUNDUCHI PWANI





Moja kati ya jamii iliyochangia kueneza uislamu katika Ukanda wa pwani ya mashariki ya Tanganyika ni Jamii ya Washirazi kuanzia maeneo ya  Zanzibar Mpaka Bagamoyo ambapo kuna sehemu mbalimbali za makumbusho ya jamii ya washirazi ambayo watu wengi hawaijui  hapa natazama makaburi ya Kunduchi ambapo watu wengi pengine hata wanaoishi Eneo hilo hawaijui historian ya  watu walioishi Eneo hilo katika Karne ya Kumi na Tatu .

Leo namuangazia Bwana Mohameda Bakari Mtumini ambaye  yeye na Mdogo wake waliishi Eneo hili na kufikia na kufikia  hapa na  nitamzungumzia zaidi  Mohamed Bakari Mtumini kiongozi wa washirazi jamii iliyoweka ngome yake katika Eneo la chuo cha Uvuvi kwa sasa au kwa wakati huo ikijulikana kama Bandari ndogo ya Salam .
Bakari Mtumini ni moja kati ya Viongozi wa mwanzo walioongoza katika Biashara mbalimbali za pembe za Ndovu,shanga,pamoja na sahani kutoka asia na afrika na  ni watu ambao wana asili ya Uajemi maeneo ya Iran na Iraq ,Mtumini alifia maeneo ya Kunduchi kwa sasa katika karne ya Kumi na Tatu na kuzikwa katika makaburi ya washirazi ambayo yapo Nyuma ya shule ya wanawake ya Kiiislamu .

Kwanini Mtumini ? Ukifika kwenye kaburi la Bwana mtumini moja kati ya viongozi waliongoza jamii ya washirazi na uenezwaji wa Dini ya  uislamu katika ukanda wa pwani ,ukifika katika kaburi utaona yafuatayo:-  kwanza likiwa limejengwa kwa mawe na kugandishwa kwa chokaa ,lakini pili  japokuwa alikuwa muislamu na kama hujuavyo makaburi ya kiislamu mengi hayajengwa lakini kaburi hili limejengwa kwa mfano wa aina yake huku likiwa limewekewa urembo na kugundishwa na vitu mbalimbali hasa alivyokuwa akivitumia na kuhusishwa navyo wakati wa ufanyaji biashara katika karne ya kumi na tatu .


Ni kaburi hili lilojengwa kwa mfumo wa kipekee tofauti na makaburi mengine yaliyopo ni mfano wa pango ambalo ni mahsusi kwa ajili ya ukumbusho wa kizazi kijacho ambapo lengo hasa lilikuwa kuonyesha umuhimu juu ya kiongozi huyu wa kiilsamu katika jamii ya washirazi .

Eneo hili la Kunduchi Chuo cha Uvuvi  halifamiki sana na wanahistoria au idara ya mambo ya kale pengine kwakuwa lipo sehemu ambayo imekuwa makazi ya watu Bila shaka hata wakazi husika wa sasa hawajui maana au historia ya Sehemu kiasi cha kupaita magofu yaani sehemu ambayo haina maana au imetelekezwa . 

Na  hii ndio sababu hata shule za karibu katika Eneo hilo hukimbilia sana katika makumbusho ya kaole bagamoyo na ya kijiji cha makumbusho yaliypo mjini na kuyaacha ya karibu ambayo yanahistoria ya kipekee pale Kunduchi .
 Sababu kuu ni idara ya mambo ya kale kuyapa kisogo mapango haya ya kale ya Kunduchi Mtongani haijulikani kabisa Pengine kwa sababu yapo Nje kabisa ya Jiji la Dar es salaam na inawezekana hakuna mawasiliano ya moja kwa moja kati ya waongoza watalii wa Eneo na watu wa idara ya Mambo ya kale.
Katika Makaburi ya Kunduchi kuna Makaburi Mengi ya kale na ya sasa ambapo kila uchao watu huendelea kuzikwa na waliowengi katika makaburi haya ni waislamu kutokana na Eneo huika la jamii iliyokuwa ikiishi hata unapofika maeneo ya kunduchi pwani jamii kubwa ya watu wanaoishi Eneo hilo ni kutoka ukanda wa pwani yaani Unguja,Pemba,na Bagamoyo sehemu ambazo washirazi walijikita sana wakiongozwa na Mohamed Bakari Mtumini.

Maoni 1 :

  1. kaburi hilo lipo kunduchi... mbna umeandika zanzibar maridhawa

    JibuFuta