Historia ya M'buyu huu wa bagamoyo ni kubwa sana ulipandwa mwaka 1868 na kasisi Anthony Horner (cssp) kwa ajili ya ufunguzi wa misheni ya Katoriki ya Bagamoyo miaka ishirini na saba baadaae yaaani mwaka 1895 Muuguzi wa kujitolea Madama Chevalier aliyekuwa akifanya kazi katika zahanati ya Zanzibar alikuwa bagamoyo kuwasaidia wauguzi walikuwa wakifanya kazi katika Zahanati ya Misheni ya Bagamoyo .
Alifunga mnyororo wa kufungia punda wake alipokuwa akija kazini lakini kutokana na kukuwa kwa M'buyu huu sehemu kubwa ya Mnyororo huu umemezwa na nyororo hiyo seheme yake ya mwsiho haioneka kwa ustadi zaidi .
Mwaka 2012 nyororo hii iliongezwa kwa mita thelathini na nne ili kuendelea kuweka historia na wakati huo mzingo wa ubuyu ulikuwa mita 13
Hiyo ni sahihi kabisa japo wengine hudhani (kimakosa kabisa!) kuwa mnyororo huo ulitumika kwa ajili ya kuwafungia watumwa!
JibuFuta