MUZIKI WA MALIMBA

MUZIKI WETU

HABARI? MPENZI MSOMAJI KARIBU KATIKA KURASA HII MAALUM KWA AJIRI YA HABARI ZIHUSUZO UTALII NA UTAMADUNI KUTOKA KATIKA VISIWA VYA MARASHI YA KARAFU ZANZIBAR ,NA MAENEO JIRANI YANAYOFANANA TABIA NA VISIWA HIVI +255 713 15 33 48

Ijumaa, 11 Septemba 2015

MSIKITI NA KANISA SEHEMU MOJA WAPI HAPO ?

Wengi wetu tunaifahamu Zanzibar kama Nchi yenye idadi kubwa ya waumini wa Dini ya  Kiislamu kuliko wakristo lakini huwezi amini japokuwa kuna  uwingi wa waislamu bado watu wameendelea kuheshimiana na kupendana .

Kuna Baadhi ya sehemu Dunia sitazitaja ni Vigumu kukuta Nyumba za Ibada za Imani Mbili Tofauti  hasa za hizi mbili uislamu na ukristo kukaa pamoja lazima watagombana kutokana na kuwa na imani kali za kidini Lakini ni tofauti katika mji wa Ston Town ambapo Msikiti na Kanisa Vipo karibu sana na hii ni historia ya kipekee inayopatikana Zanzibar katika mji maarufu wa stone Town .

Labda unaweza kudhani ni uongo ukihisi hivyo panda Boti au Ndege fika stone town ujionee na kila mmoja anaheshimu ibada ya mwenzake hakika ni sehemu ya kihistoria sio rahisi hata kidogo kuamini jambo kama hili linaweza kutokea lakini ndivyo ilivyo katika nchi ya Zanzibar .

Nchi iliyoungana na Tanganyika na Kuuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .Wapi kama Zanzibar

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni