Ijapokuwa nilizaliwa Eneo hili na nakuishi hapa kwa miaka
kadhaa sikuweza kujua kuwa Eneo nililoishi Mwanzo linahistoria ya kipekeee kama
unavyoona pichani .
Kijiji cha Kunduchi kilichopo Nje kidogo ya Jiji la Dar Es salaam mashariki
wa Mwa Tanzania karibu kabisa na kituo cha Uvuvi Kunduchi kwa sasa na jinsi kilivyo huwezi kufikili au kuamini kua jamii
ya watu kutoka Huba ya uajemi ( Iran) iliwahi kuishi katika Eneo hilo na kuanza kujulikana kama Makaburi
ya Washirazi .
Jambo kubwa ambalo sasa linaweza kuonekana kama la mzaha ni
kuwa kijiji hiki ni kijiji cha Kiiislamu ambapo ndani ya Eneo hili kuna
makaburi mengi lakini kikubwa zaidi ni msikiti uliojengwa katika Karne ya Kumi
na Tano kwa kutumia mawe ya matumbawe
yaliyokuwa yakipatikana Baharini ambayo yalikuwa na kazi ya kutunzia Mazalia
ya Samaki vile vile katika ujenzi huo walijengea kwa miti
iliyokuwa ikiitwa mitandaa miti hiyo ilitumika kusimamishia ukuta ili isibomoke
lakini kwa Bahati Mbaya au Nzuri msikiti huu haukuweza kumalizika kwa kuwekwa paa na kama
ujuavyo ni kuwa msikiti unakuwa na Nguzo na nane lakini baadhi ya Nguzo za
Msikiti huu zimeanguka na kupotea.
Jambo jingine katika msikiti huu uliojengwa karne ya kumi na
Tano hata kuta zake zimekwisha bomoka na kutishia kupotea kwa historia ya
msikiti na pembeni ya msikiti kuna kaburi la Imamu wa msikiti huo ambaye
inasemekana jina lake alikuwa akiitwa Mtumwa wa Nyuki ingawa bado hakujawa na
uhakika wa jina kama ni sahihi au sio sahihi.
Kama nilivyo kueleza mwanzo msikiti huu ulijengwa na
washirazi kwa ibada yao ya Dini ya kiislamu na pia palikuwa na kisima ambacho kilikuwa
kinahifadhi maji ya kuwekea Udhu lakini mpaka leo hakijaweza julikana kuwa kilikuwa
wapi katika Eneo hili kwani baadhi ya
Eneo hilo kumeingiliwa kwa kujengwa shule ambayo ni ya kiislamu .
Katika kuboresha historia zipo Baadhi ya sehemu ambazo
zimelekebishwa kwa saruji katika miaka ya 1964 katika historia ya makaburi hayo yaliyojengwa kwa kutumia chokaa kwa upande mwingine kuna fanyika utafiti
unafanywa ili kujua washirazi hawa waliishi wapi? kwa maana ilikuwa ni Bandari
Ndogo kwa wafanyabiashara kutoka Uajemi na sehemu za Asia wakifanya Biashara za
Ndovu ,Shanga na nyinginezo zilizohusu ukanda wa pwani ya wakati huo ikiitwa
Tanganyika.
Lakini ki mandhari kunaonekana kuwa kabla ya hawa washirazi
hawajafika katika Eneo hili kulikuwa na jamii iliyokuwa iikiiishi hapo
haijajulikana kuwa ni jamii ya watu gani iliyokuwa ikiiishi katika Eneo hili la
Kunduchi pwani lakini hata leo hi asilimia kubwa ya watu wanaoishi Maeneo ya
Eneo hilo ni waislamu na kuifanya historia ya Eneo kuendelea kuonekana kuwa ya
Umuhimu zaidi katika Eneo la kunduchi pwani ni Historia iliyojificha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni