MUZIKI WA MALIMBA

MUZIKI WETU

HABARI? MPENZI MSOMAJI KARIBU KATIKA KURASA HII MAALUM KWA AJIRI YA HABARI ZIHUSUZO UTALII NA UTAMADUNI KUTOKA KATIKA VISIWA VYA MARASHI YA KARAFU ZANZIBAR ,NA MAENEO JIRANI YANAYOFANANA TABIA NA VISIWA HIVI +255 713 15 33 48

Jumatano, 1 Juni 2022

TAARIFA KWA UMMA WATALII WALIOINGIA NCHINI, KIPINDI CHA JANUARI - APRILI, 2022

 

Taarifa ya mwenendo wa watalii waliongia nchini ni miongoni mwa taarifa za muda
mfupi (high-frequency data) zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa mujibu
wa Sheria ya Takwimu SURA 351.
Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Januari - April 2022
Katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Aprili 2022, idadi ya watalii 367,632
kutoka nje ya nchi walitembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikilinganishwa na
watalii 275,097 walioingia nchini kipindi kama hicho mwaka 2021. Hili ni ongezeko la
watalii 92,535 sawa na asilimia 33.6 (Jedwali Na. 1). Kati ya watalii 367,632 walioingia
nchini, watalii 124,212 waliingia nchini kupitia Zanzibar ambao ni sawa na asilimia
33.8 ya watalii wote.

 
Watalii walioingia nchini mwezi Aprili 2022, waliongezeka hadi 78,784 kutoka watalii
43,966 walioingia nchini mwezi Aprili 2021. Idadi ya watalii walioongezeka walikuwa
34,818 sawa na asilimia 79.2. Ongezeko hilo limetokana na nchi nyingi duniani
kuondoa zuio la kusafiri kufuatia kupungua kwa hali ya maambukizi ya UVIKO-19
na juhudi za Serikali kuendelea kutangaza vivutio vya utalii nchini.
Jedwali Na. 1: Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Kuanzia Januari Hadi Aprili 2022
2021 2022 Ongezeko Badiliko (%)
Januari 79,116 94,128 15,012 19.0
Februari 79,730 100,936 21,206 26.6
Machi 72,285 93,784 21,499 29.7
Aprili 43,966 78,784 34,818 79.2
Jumla 275,097 367,632 92,535 33.6
Chanzo: Idara ya Uhamiaji, 2022
Idadi ya Watalii Walioingia Nchini Kabla na Baada ya UVIKO-19
Idadi ya watalii walioingia nchini mwaka 2019 walikuwa 1,510,151 ambapo idadi
kubwa zaidi ya watalii 160,296 waliingia nchini mwezi Desemba 2019. Baada ya dunia
kukumbwa na UVIKO-19, nchi nyingi ziliweka vikwazo vya kusafiri vilivyosababisha
idadi ya watalii walioingia nchini kupungua hadi 620,867 mwaka 2020 ambapo idadi
ndogo zaidi ya watalii 7,105 waliiingia nchini mwezi Aprili 2020. Mwaka 2021, idadi
ya watalii walioingia nchini iliongezeka hadi 922,692, sawa na asilimia 48.6.

Kumb. Na. BA.275/376/01/20 Tarehe: 18 Mei, 2022
Mawasiliano yote yafanyike kupitia kwa Mtakwimu Mkuu wa Serikali
Matarajio ya Idadi ya Watalii Wanaoingia Nchini
Idadi ya watalii wanaotarajiwa kuingia nchini itaongezeka zaidi ya idadi iliyokuwepo
kabla ya UVIKO-19 kutokana na juhudi mbalimbali za Serikali za kutangaza vivutio
vya utalii ambavyo ni pamoja na mbuga za wanyama, fukwe za bahari, Mlima
Kilimanjaro, uwindaji na utalii wa kitamaduni. Aidha, kukamilika na kuanza
kurushwa kwa filamu ya Tanzania, the Royal Tour iliyozinduliwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imeiwezesha
Dunia kuitambua Tanzania. Kuongezeka kwa viwango vya ukuaji wa shughuli za
uchumi zinazohusiana na sekta ya utalii zinazojumuisha Sanaa na Burudani (asilimia
11.7) na Malazi na Huduma za Chakula (asilimia 11.3) ni miongoni mwa viashiria
vinavyoonesha kuendelea kuimarika kwa sekta ya utalii nchini.

 

Jumanne, 31 Mei 2022

RAIS SAMIA AMUOMBA Juliano Belletti KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII KABLA HAJAONDOKA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuomba Mchezaji wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil ,Barcelona na Chelsea  kusalia Nchini  kwa Siku Kadhaa ili Apate Nafasi ya Kwenda Kutizama Vivutio Vya Utalii Vilivyopo Hapa Nchini .


Rais Samia Ametoa Ombi Hilo wakati wa Akipokea Kombe Halisi la Dunia linalofanya Ziara ya Siku mbili  ikiwa ni Kiashiria cha Hamasa la Kombe la Dunia litalofanyika Nchini Qatar Mwezi November Mwaka Huu ambapo hii ni Mara ya pili kufanya Ziara Hiyo Mara kwanza lilipokewa na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu Nne Jakaya Mrisho Kikwete .

Rais Samia Amemwambia Belleti '' Belleti you can spare some Days to Visit Serengeti so That you can see the wonders of Tanzania .

Akimwambia Kuwa unaweza Kusalia hapa Nchini kwa siku Kadhaa ili ujionee Maajabu ya Vivutio vya Utalii vya Tanzania kwani Ukitoka na Kurudi tena Gharama zinaweza kuwa Kubwa .

 

 

 

Julioni Belleti ambaye Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA)  ni Moja kati ya Wachezaji waliokuwemo Kwenye Kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil kilichotwaa ubingwa kwa Mara tano katika Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika kwa Mashirikiano kati ya korea ya Kusini na Japan 2002 .

Pia amewahi Kutwaa Ubaingwa wa Ulaya akiwa na klabu cha Barcelona cha Uispani na amewahi Pia Kucheza katika Klabu cha Chelsea kinachoshiriki ligi ya kuu ya Nchini uingereza  .

Aidha Rais Samia  amegusia mambo mbalimbali Ikiwemo kuongeza bidii katika Maandalizi ya timu za Taifa ambazo  serikali imekwisha Aanzisha mfumo Maalumu wa Timu ya Taifa ya Tanzania .

Kikombe Hicho kinazuru Nchini Nane  katika Bara afrika  katika Hizo Nne hazijafuzu kucheza kombe hilo la  Daunia  .

Jumatano, 9 Machi 2016

MANGAPWANI(PANGO LA KUHIFADHIA WATUMWA ZNZ)


 

Mangapwani (Maana yake ni Ufukwe wa kiarabu ') Ni pango  la kuhifadhia watumwa lipo kilometa 20km kaskazini mwa Mji wa Zanzibar. Eneo hilo la kufahidhia Watumwa ambalo limejengwa kwa kutumia mawe yaliyo katwa katika mwamba huku likiwa na mlango mdogo sana wa kuingilia  ambamo ndani kuna maji safi   lipo huko kisiwani Zanzibar . kutokana na uoto wa asili ambao umesababishwa na Unyevu Unyevu kulisababisha kuota kwa nyasi kiasi ambacho kilisababisha Pango hilo kusahaulika  .

Baadae Pango hili lilimilikiwa na Mwaarabu aliyejuilikana kwa jina la  Hamed Salim el Hathy  ambae alimiliki watumwa wengi zaidi katika Pango hilo . Katika zama hizi ,Pango Hili liligunduliwa na kijana mdogo aliyekuwa akitafuta mbuzi wake baada ya kupotea  Na hapo ndipo watu wa Eneo hilo wakaanza kutumia tena maji ya Eneo hilo, na Bwa  Hamed Salim alikuwa akitumia maji hayo kwa matumizi binasfi .
Imewakadiliwa kuwa Eneo hilo lilikuwa likihifadhia watumwa tangu Biashara hiyo ilipopigwa marufuku mwaka  1873.

Watu wengi huenda kutembelea Eneo hilo visiwani Zanbzibar , Kwa kutumia Usafiri Binafsi eidha kwa baskeli au gari na pikipiki pia. Aidha yapo magari ambayo hufanya safari kutoka Zanzibar Mjini Hadi Mangapwani , japokuwa huduma hizo sio za mara kwa mara . na ili kufika huko magari mengi hupitia njia Bububu hadi Chuini, na baadae kufuata uelekeo wa Bumbwini. ni kilometa sita 6km, kutumia njia hiyo kufika Kijiji cha Mangapwani ,  

Sehemu ya ndani ya Kuhifadhia watumwa ya  Mangapwani ipo kilometa Kadhaa kutoka kwenye Mwamba wa  Bahari ya Hindi   Japokuwa wakati mwingine panaitwa  (Pango la watumwa),Ni Eneo lilojengwa juu ya mwamba huku likiwa na paa kwa juu .

Lilijengwa maarumu kwa kuhifadhia watumwa na Ujenzi wa Eneo hilo ulibuniwa na Mohammed bin Nassor Al-Alwi, moja katika ya wafanya biashara Muhimu wa watumwa  . Boti kutoka Tanganyika ambalo lilikuwa Koroni la Kijerumani zilikuwa zikibeba watumwa  na kuwapeleka katika Mashua ambazo ziliwasafirisha hadi 

hadi kwenye cha maji mengi  na Kwenda Zanzibar  ili kwenda kuuzwa na kufanya shughuri mbalimbali za kilimo .
Pango hilo linafikiliwa ya kwamba baada ya mwaka 1873, wakati  Sultan Barghash alipotia saini usitishwaji wa Biashara ya watumwa Anglo–Zanzibari Treaty   Eneo hili  bado lilitumika kuhifadhia watumwa kinyemela na kwa miaka mingi .


Jumamosi, 9 Januari 2016

ROMAN CATHORIC ZANZIBAR


Hii ni moja kati ya maeneo ya Zamani ya Mji wa Zanzibar katika kisiwa cha unguja ndani ya Mji mkongwe  (Stone town) sehemu iliyopo ndani kidogo ya Bahari ya Hindi na Ni rahisi sana ukiwa katika Eneo hilo kujionea Mandhari nzuri ya Mji mkongwe  
Na ni eneo zuri zaidi kwa wafanya Biashara kufanya biashara zao katika eneo hilo kwani watalii wengi hujivinjari sehemu hiyo na ukiwa unatembea ni vigumu kupotea katika eneo kwani limekaa katika mpangilio unaostahili .

BEIT-EL -AJAIB LINAPOKOSA MATUNZO


Hili ni jengo lenye historia kubwa sana katika visiwa vya Unguja lakini ni wazi linakosa mwangalizi wa uhakika licha ya kuingizia kisiwa cha unguja fedha nyingi sana katika nyanja ya utalii lakini bado kimekosa uangalizi unaostahili na linazidi kuharibika kila uchao .

Jumanne, 22 Septemba 2015

KIFO CHA MWANAMWALI KARNE YA 15





Moja kati ya mambo mengi na ya msingi katika miaka ya leo ni watu kufanyiwa maziko ya kifahari kanakwamba vitu wanavyokwenda kuzikwa  navyo  watavitumia huko waendako na wengine wamekuwa wakilaani utaratibu huo kutokana na imani zao binafsi na maisha ya kileo lakini  kumbe tabia hii haikuanza katika karne ishirini na moja imeanza katika karne ya kumi na tano miaka takriban mia tano na ushehe hivi imepita ambapo jamii za wakati huo zilikuwa zikifanya haya yanayofanyika leo.

Leo tunamtazama Binti wa Kishirazi aitwae Mwanamwali Binti huyu aliposwa katika Karne ya Kumi na tano na hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa Binti huyo alikuwa na Umri wa Miaka Mingapi katika maisha yake ya kuishi Duniani Kaburi la mwanamwali lipo katika Kijiji cha Kunduchi pwani kijiji ambacho kinahistoria kubwa zaidi ya Uislamu.

Mwanamwali Baada ya kuposwa alifariki Dunia siku chache baadae na ndoa yake haikufungwa japokuwa mahali ilikuwa tayari imekwisha kutolewa  kwanini Mwanamwali ? Kaburi la Binti huyu wa kishirazi limejengwa kwa mawe ya matumbawe ambayo hata leo bado yapo Tangu karne ya Kumi na Tano kikubwa zaidi na cha ajabu ni kuwa waliamua kuweka vitu alivyolipiwa kama mahali wakati anaposwa ambapo vimegandanishwa kwa kutumia chokaa ya moto na vipo hadi leo hii, ni kaburi lililojengwa mfano wa Nyumba na limerembwa utadhani kulikuwa na mashine za kufanyia kazi hiyo  wakati huo .

Hii ni moja kati ya historia kubwa ambayo ipo kunduchi chuo cha Uvuvi ambapo watu wengi hawaitilii maanani pengine kwa kutojua umuhimu au maana ya historia za aina hii na kuna vitu vingi sana vya kustaajabisha katika makuburi haya  pengine inawezekana yakawa ndio makaburi yenye Gharama zaidi kuliko hata ya sasa kiuhalisia Tabia hizi zimekuwa zikijirudia rudia katika maisha ya wanadamu.